價格:免費
更新日期:2017-11-17
檔案大小:63M
目前版本:2
版本需求:Android 4.1 以上版本
官方網站:http://curiouslearning.org
Email:info@curiouslearning.org
聯絡地址:Curious Learning 34A Walker St Cambridge, MA 02138
Mlishe Zimwi humfundisha mwanao misingi ya kusoma . Kusanya mayai ya zimwi na umlishe herufi ili akue na wawe marafiki wapya.
MLISHE ZIMWI NI NINI?
Mlishe zimwi hutumia mbinu zilizo thibitishwa za “ Cheza kujifunza” kuwashirikisha watoto na kuwasaidia watoto kujifunza kusoma , Watoto hufurahia kukusanya na kukuza mazimwi yao ya kufuga huku wakijifunza kanuni za kusoma.
NI BURE KUPAKUA , HAINA MATANGAZO , HAINA MANUNUZI YA NDANI YA APP
Maudhui yote ni bure kwa asilimia 100, imetengenezwa na Literacy nonprofits Curious Learning, CET na App Factory
VIPENGELE VYA MCHEZO AMBAZO HUCHOCHEA UJUZI WA KUSOMA
•Inafurahisha na kushirikisha
•Michezo ya kufuatilia herufi ili kusaidia kusoma na kuandika
•Michezo ya kukalili misamiati
•Michezo ya changamoto za kusikiliza sauti
•Ripoti ya maendeleo kwa mzazi
•Inaweza kuchezwa na zaidi ya mtu mmoja
•Mizimwi inayokusanyika , kukua na kufurahisha
•Imeundwa kukuza stadi za kijamii
•Hamna manunuzi ya ndani ya App
•Hamna matangazo
•Haiitaji maunganishi ya Internet
IMETENGENEZWA NA WATAALAMU KWA AJILI YA MWANAO
Huu mchezo umetokana na miaka ya utafiti na uzoefu katika sayansi ya kusoma na kuandika . Imeundwa na mbinu muhimu katika kusoma na kuandika , pamoja na uelewa wa kifonolojia , utambuzi wa herufi , misamiati na kusoma kwa kuona ili watoto waweje kujijengea msingi imara wa kusoma . Imeunda katika mtazamo wa kuwajali na kuwalea kikundi cha zimwi , imeunda ili kuhamasisha kuwajali watu wengine , uvumilivu na kuwa na mbinu za kijamii kwa watoto.
SISI NI NANI?
Mlishe zimwi imedhaminiwa na wizara ya mambo ya nje ya Norway kama moja ya mikakati ya EduApp4syria-competition . App ya awali ya kiarabu ilitengenezwa kwa ushirikishi kati ya Apps Factory , CET – The Center for Educational Technology na IRC – The International Rescue Committee.
Mlishe zimwi ili badilishwa kwa Kiswahili na Curious Learning , shirika lisilo la kifaida linalojidhatiti katika kueneza upatikani wa maudhui ya kusoma na kuandika kwa ajili ya mtu yeyote atakae ihitaji . Sisi ni timu ya wafanya uchunguzi , waendelezi na wafundishaji tuliojidhatiti kuwapa watoto duniani kote elimu ya kusoma na kuandika katika lugha yao mama kutokana na ushahidi wa data – na tunafanya kazi kuleta Mlishe Zimwi App kwa lugha zaidi ya 100.